Monday 18 May 2015

Barcelona bingwa La Liga

Barcelona bingwa La Liga


Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi akishangilia goli aliloifungia timu yake na kuipa ubingwa wa ligi ya Hispania (La liga)
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi akishangilia goli aliloifungia timu yake na kuipa ubingwa wa ligi ya Hispania (La liga)
Lionel Messi amewapa Barcelona ubingwa wa La Liga msimu wa 2014-2015 baada ya kuifungia timu yake bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Atletico Madrid kwenye uwanja wa Vicente Calderon.
Messi amefunga goli hilo katika dakika ya 65 akimalizia pasi ya Pedro Rodriguez.
Kwa matokeo hayo Barcelona wamefikisha pointi 93 baada ya kushuka dimbani mara 37 na wamebakiza mechi moja.
Real Madrid wameshinda magoli 4-1 kwenye mchezo wa leo dhidi ya Espanyol na kufikisha pointi 89 baada ya mechi 37 walizocheza.
Kwa maana hiyo wakishinda mechi ya mwisho watafikisha pointi 92 ambazo tayari zimeshavukwa na Barcelona.
Inawezekana msimu ukawa mkubwa kwa Barcelona, leo wameshatwaa taji la ligi kuu (La Liga) na watacheza fainali mbili, ligi ya mabingwa barani Ulaya na kombe la mfalme ‘Copa del Rey’.
Mbali na machungu ya timu yake kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya katikati ya wiki hii na leo kukosa ubingwa wa La Liga, mshambuliaji hatari wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amefunga magoli matatu peke yake ‘hat-trick’ katika ushindi wa Madrid wa goli 4-1.
Ronaldo amefunga magoli hayo katika dakika ya 59, 83 na 90. Goli lingine limefungwa na Marcelo dakika ya 79 wakati goli la kufutia machozi kwa Espanyol limefungwa na Cristian Stuani dakika ya 73.

clouds stream