Sunday 3 May 2015

Urais 2015: Kamati kuu CHADEMA yajichimbia jijini Dar es salaam

Urais 2015: Kamati kuu CHADEMA yajichimbia jijini Dar es salaam



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa.
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA   chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, inatarajia   kujichimbia   jijini Dar es samaa  kuanzia  Mei 3-4 kujadili uchaguzi mkuu wa rais na wabunge unaotarajia kufanyika wiki ya mwisho ya mwezi oktoba.
Kwa  mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa CHADEMA  Tumaini Makene  imebanisha kwamba katika kikao hicho cha siku mbili, pamoja na masuala mengine ya kitaifa kuhusu hali ya kisiasa nchini kwa ujumla na mengine mahsusi yanayohusu uendeshaji wa chama, KK itapokea taarifa, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu;
  1. Maandalizi ya Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
  2. Taarifa ya ziara ya mafunzo kwa timu za kampeni, viongozi wa serikali za mitaa na chama, kukiandaa chama kushinda
    dola na kuongoza serikali baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
  3. Taarifa za utendaji wa chama kupitia kanda zote 10, Tanganyika na Zanzibar.
  4. Taarifa ya maendeleo ya mikakati ya kushiriki uchaguzi mkuu kwa kushirikiana na vyama 4 vinavyounda UKAWA.
  5. Taarifa za mwenendo wa shughuli ya uandikishaji wa wapiga kura (upya) katika daftari la kudumu kwa teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) na hatma ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Hata hivyo, hivi karibuni chama hicho kupitia umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA wameitaka tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kutoa ratiba nzima ya uchaguzi mkuu kwa mwaka  huu 2015.

clouds stream