Tuesday 26 May 2015

NEC yatoa ratiba Uchaguzi mkuu 2015

NEC yatoa ratiba Uchaguzi mkuu 2015

Tarehe May 25, 2015
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania, Jaji Damian Lubuva.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania, Jaji Damian Lubuva.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa rasmi  ratiba kwa vyama vya Siasa na wananchi wote itakayotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali  unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo  Jaji wa Rufaa (Mst.) Damian Lubuva imesema kuwa kwa Mamlaka waliyopewa kwa mujibu wa vifungu vya 35B(1), (3) (a), 37 (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,  Sura ya 343, shughuli za uchaguzi zinatarajia kuanza hivi karibuni.
Uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani unatarajia kufanyika Agosti 21, 2015, na  kampeni za Uchaguzi kwa wagombea hao zitatarajia kuanza Agosti 22 mpaka – Oktoba 24 mwaka huu.
Siku ya kupiga kura kwa wananchi wote inatarajiwa kuwa Oktoba 25, 2015 kwa wale waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.

clouds stream