Tuesday 26 May 2015

Burkina Faso: Madaktari kupima DNA Mwili wa aliyekuwa Rais Thomas Sankara

Burkina Faso: Madaktari kupima DNA Mwili wa aliyekuwa Rais Thomas Sankara

Tarehe May 26, 2015
 Thomas Sankara enzi ya uhai wake.
Thomas Sankara enzi ya uhai wake.
Ripoti za mahakama nchini Burkina Faso zinasema kuwa mwili ambao unaokisiwa kuwa wa raisi wa zamani aliyeuawa Thomas Sankara utafukuliwa hii leo katika jaribio la kutaka kubainisha ikiwa ni wake.
Familia na marafiki wa rais Sankara wamekuwa na shauku ya kutaka kufahamu  iwapo mabaki hayo ni yake.
Bwana Sankara aliuawa wakati wa mapinduzi mwaka 1987. Sankara alichukuwa uongozi baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1983.
Sankara alipinduliwa na Blaise Compaore ambaye aliitawala Burkina Faso hadi mwaka uliopita alipolazimishwa kuondoka na maandamano makubwa katika mji mkuu wa wa nchi hiyo Ouagadougou
Madaktari wawili kutoka Burkina Faso na mmoja kutoka Ufaransa watachukua chembechembe za mwili huo na kuipima wakitumia mashine na mbinu za kisasa za DNA ilikubaini kikamilifu iwapo inahusiana na mwili wa Sankara.
Miili mingine 12 ya wafuasi wake waliouawa pamoja naye pia itafukuliwa.
Mabaki hayo ya Sankara yamezikwa katika makaburi ya Dagnoen katika mji mkuu wa Ouagadougou.

clouds stream