Monday 4 May 2015

Chelsea bingwa Uingereza

helsea bingwa Uingereza



Eden Hazard akishangili pamoja na Nemanja Matic
Eden Hazard akishangili pamoja na Nemanja Matic
Chelsea ndio mabingwa wapya wa ligi kuu nchini Uingereza mara baada ya kuichapa timu ya Crystal Palace kwa bao 1-0 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Stamford bridge jijini London.
Bao la Chelsea limefungwa na Eden Hazard katika dakika ya 45 kwa kichwa baada ya hapo awali kipa kupangua mkwaju wa penati kasha Hazard baadae kuunganisha kwa mara nyingine tena.
Eden Hazard akipiga mpira kwa kichwa kuifungia goli timu yake
Eden Hazard akipiga mpira kwa kichwa kuifungia goli timu yake
Ushindi huo umeipeleka Chelsea pointi 16 zaidi ya Arsenal ambao hata hivyo wana michezo mitano kibindoni.
Lakini hata Arsenal na Man City wakishinda michezo yao yote iliyosalia bado hawataweza kuwafikia Chelsea.
Hazard akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga goli
Hazard akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga goli
Hii ni mara ya tatu sasa kwa Mourinho kushinda kombe hilo akiwa na Chelsea na ni mara ya kwanza kwake tangu arudi tena klabuni hapo mwaka 2013.
Chelsea sasa watakuwa wamechukua kombe hilo kwa mara ya tano tangu klabu hiyo kuanzishwa.

clouds stream