Wednesday 13 May 2015

Barcelona yatinga fainali klabu bingwa Ulaya

Barcelona yatinga fainali klabu bingwa Ulaya



Wachezaji wa Barcelona wakishangilia baada ya Neynar Jr kuifungia goli timu yao
Wachezaji wa Barcelona wakishangilia baada ya Neynar Jr kuifungia goli timu yao
Barcelona imefuzu kucheza fainali ya klabu bingwa Ulaya licha ya kupoteza mchezo wake wa nusu fainali ya pili dhidi ya Bayern Munich kwa kufungwa goli 3-2 mchezo uliopigwa kwenye dimba la Alianz Arena, Ujerumani.
Bayern Munich ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la mapema kupitia kwa beki wao Medhi Benatia lakini Neymar Jr alifunga magoli mawili na kuifanya Barcelona imalize kipindi cha kwanza ikiwa mbele kwa magoli 2-1.
Kipindi cha pili Bayern ilibadilika na kucheza mpira wa pasi nyingi uliowachanganya wapinzani wao na kufanikiwa kusawazisha goli kupitia kwa mshambuliaji wao Robert Lewandowski kabla ya Thomas Muller hajafunga goli la tatu na la ushindi kwa upande wa Bayern Munich.
Ushindi huo haukuisaidia Bayern kwasababu tayari ilishapoteza mchezo wake wa kwanza ikiwa ugenini kwa kukubali kipigo cha goli 3-0 kwenye uwanja wa Nou Camp juma lililopita, leo ilikuwa inahitaji ushindi wa goli 3-0 ili mchezo uongezwe dakika 30 au ushindi wa goli 4-0 ili ifuzu moja kwa moja.
Matokeo hayo yanaifanya Barcelona kusonga mbele kwenye hatua ya fainali kwa wastani wa magoli 5-3 na inasubiri mshindi wa mechi kati ya Real Madrid dhidi ya Juventus ili kujua ni timu ipi kati ya hizo mbili watakutana nayo kwenye mchezo wa fainali.

clouds stream