Tuesday 26 May 2015

Lowassa alipua upya sakata la Richmond, alia na Mwakyembe

Lowassa alipua upya sakata la Richmond, alia na Mwakyembe

Tarehe May 25, 2015
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa.
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa.
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa  ameibuka kwa mara ya kwanza na  kuzungumzia sakata la Richmond lililopelekea kujiuzulu cheo cha Uwaziri mkuu febriari 7 mwaka 2008.
Akizungumza na Wahariri leo nyumbani kwake mkoani Dodoma Edward Lowassa amesema kwamba  hausiki  kabisa na sakata ka Richmond na ndio sababu hata kamati a  Mwakyembe haikuona sababu ya  kumhoji.
Katika mkutano wake na Waandishi wa Habari akiwa   ameambatana na Nazir Kalamagi, Peter Selukamba, Diana Chilolo, Hussein Bashe ikiwa ni baadhi  ya  walio  athirika kutokana na sakata la Richmond. Katika mkutano huo pia  amemtangaza  Elizabeth Msoki kuwa mkurugenzi wa  mahusiano na Mawasiliano katika timu yake ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.
Ameongeza kuwa    cheo cha uwaziri mkuu ndio lilikuwa  lengo la kamati ya mwakyembe na Spika wa Bunge wa  wakati huo ambaye alikuwa ni Samweli Sitta. Hicho sio kikwaz kwake katika  safari yake  ya kuingia ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua huku akiahidi kuchukua muda mrefu zaidi kulizungumzia sakata hili hususani mwishoni mwa wiki hii mkoani Arusha.
Lowassa alijiuzulu februari 7 mwaka 2008 kutokana na madai ya  kuhusika ktika kashfa ya kuibeba kampuni ya Richmond Development (LLC) ya nchini Marekani katika mchakato wa upatikanaji wa zabuni ya umeme wa dharura hapa nchini.
Akizungumzia malengo yake Lowassa amesema serikali ya Jakaya  ilikosea kuanza kilimo na kuweka kando elimu huku akisisitiza sera yake itakuwa ni elimu kwanza.
Kwa upande wa Pesa  za kampeni amesema anapata kutokana na michango  ya rafiki zake na ataendelea na kupata michango hiyo.
Alipoulizwa kuhusu mpango wa kuhama  Chama chake  endapo atatatoswa  na kamati kuu (CCM) amesema asiyempenda  ndani ya  chama   hicho atahama yeye kwani  yeye ana uhakika wa kupata nafasi ya kuwania Urais huku akisisitiza kuwa hatalipa kisasi kwa jambo lolote lililomtokea katika safari yake ya kisiasa  ikiwemo sakata la Richmond.
Hata hivyo amesema Arusha itwaka moto tarehe 30 mwezi huu na kuwataka watanzania kutega sikio kwani ata aanika kila jambo kuhusu mustakabali  wa nchi hii na mipango yake ya kuinua nchi kuichumi katika miaka kumi  ijayo.

clouds stream