Tuesday 26 May 2015

Dkt.Kikwete amteua mkuu mpya wa Wilaya na kuwahamisha wengine 10

Dkt.Kikwete amteua mkuu mpya wa Wilaya na kuwahamisha wengine 10

Tarehe May 26, 2015
Rais Jakaya Kikwete atua mkuu wa wilaya mpya.
Rais Jakaya Kikwete atua mkuu wa wilaya mpya.
Rais Jakaya Kikwete  amemteua Bw.  Antony Peter mavunde kuwa mkuu wa wilaya ya  Mpwapwa mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imebainisha kwamba  licha ya kumteua mkuu wa wilaya mpya mmoja   pia   awahamisha wakuu wa wilaya wengine 10 kwa lengo la kuongeza ufanisi katika wilaya mbalimbali nchini.
Katika mabadiliko hayo,Rais kikwete amemhamisha Luteni Edward ole Lenga kutoka  wilaya ya Mkalama mkoni Singida kwenda kuwa mkuu wa wilaya  mpya ya  Kyerwa mkoani Kagera. Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni kanali benedict Kulikela kitenga ambaye alifariki dunia aprili 20 mwaka huu.
Wengine ni Elizabeth Chalamila Mkwasa kutoka wilaya ya Dodoma kwenda  wilaya ya  Mvomero mkoa wa  Morogoro. Dkt Jasmine Tisike kutoka wilaya ya Mpwapwa  kwenda  Dodoma. Agnes Elias Hokololo kutoka wilaya  ya Namtumbo  mkoani Ruvuma kwenda wilaya ya Tunduru, Fadhili Nkurlu kutoka wilaya ya Misenyi mkoani kagera kwenda  wilaya ya mkalama.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa  Chande Bakari Nalicho amehamishwa  kutoka wilaya ya  Tunduru kwenda Wilaya  ya  Namtumbo, Festo Shem Kiswaga kutoka wilaya ya  Mvomero kwenda Misenyi , Darry Ibrahim Rwegasira kutoka Karagwe mkoani Kagera kwenda  wilaya ya biharamulo mkoani humo humo.
Elias Choro John Tarimo  amehamishwa  kutoka  wilaya ya Biharamulo kwenda wilaya ya  Chunya  mkoani  mbeya   pamoja  na Deodatus   Lukasi Kinwiro kutoka wilaya ya Chunya kwenda wilaya ya  Karagwe mkoani Kagera.

clouds stream