Monday 4 May 2015

Wananchi 700 waokolewa kambi ya Boko Haram


Wananchi 700 waokolewa kambi ya Boko Haram




Jeshi la CHAD nchini Nigeria.
Jeshi la CHAD nchini Nigeria.
Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaokoa zaidi ya watu mia saba katika kipindi cha wiki moja iliyopita wakati wa mapigano makali yanayoendelea dhidi ya Boko Haram. Mateka mia tatu wameokolewa kutoka msitu wa Sambisa na kupelekwa katika kambi ya serikali.
Wakizungumzia mateso waliyoyapata kutoka kundi la Boko Haram baadhi ya mateka wamesema kwamba baadhi yao waliuawa kwa kupigwa mawe na wapiganaji wa Boko Haram wakati jeshi lilipokaribia kuwaokoa.
Mwanamke mmoja ambaye alijifungua akiwa mateka ameelezea namna wapiganaji hao walivyomkata koo mumewe wake mbele yake, kabla mwanamke huyo kutenganishwa na watoto wake wengine watatu.
Katika hatua nyingine  wengi wa wananchi waliokolewa  katika kambi ya serikali  imebainika kuwa wengi wa watoto waliokolewa walikuwa wanaugua utapiamlo mkali.

clouds stream