Tuesday 26 May 2015

CCM yatoa ratiba uchukuaji fomu za Urais

CCM yatoa ratiba uchukuaji fomu za Urais

Tarehe May 25, 2015
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Kikwete Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Kikwete Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Kikao cha halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi (NEC)  imetoa  ratiba ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi  huku nafasi ya urais wa jamuhuri ya muungano wagombea wakitakiwa kuchukua fomu kuanzia June tatu mpaka Julai mbili mwaka huu.
Akizungumzia ratiba hiyo  katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye amesema wagombea urais wa jamuhuri ya muungano na ule wa Zanzibar watatakiwa kuchukua fomu kuanzia tarehe tatu june na kuzirudisha tarehe 2 julai.
Katika kipindi hicho pamoja na mambo mengine watatakiwa kutafuta wadhamini wasipopungua 450 kwa nafasi ya jamuhuri kutoka Mikoa 15 mitatu kati yake iwe Zanzibar na urais wa Zanzibar wadhamini 250 kutoka mikoa mitatu ya Zanzibar.
Mara baada ya zoezi hilo litafuatiwa na vikao mbalimbali vya uchujaji wa majina ya wagombea kwa kuanza na kikao cha kamati ya usalama na maadili tarehe 8/7 kikifuatiwa na kikao cha kamati kuu tarehe 9/7 halafu halmashauri kuu ya CCM NEC itakayotoa jina la mgombea wa urais tarehe 10/7 na kisha mkutano mkuu utakaofanyika tarehe 12/13 mwezi jully.
Kwa upande wa  nafasi za ubunge na udiwani na baraza la wawakilishi wagombea watatakiwa kuchukua fomu kuanzia tarehe 15-19 mwezi jully ambapo kampeni za ushawishi kwa wanachama kwenye matawi zitafanyika kuanzia tarehe 20 mpaka 31 jully.
Kura za maoni kwa ajili ya kuwapata wagombea katika ngazi hizo zitapigwa sambamaba tarehe 1/08 2015 huku wagombea wote wakitakiwa kuzingatia maelekezo ya kanuni na taratibu za chama hicho.

clouds stream