Wednesday 13 May 2015

Rais Nkurunzinza ”apinduliwa” Burundi

Rais Nkurunzinza ”apinduliwa” Burundi


Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Vurugu nchini Burundi.
Vurugu nchini Burundi.
Meja Generali Niyombareh  aliyetimuliwa nchini Burundi  ametangaza rasmi kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi.
Amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa  awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
Wakati akitangaza uamuzi huo Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la nchini Burundi.
Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpito.
Habari kutoka Burundi zimebainisha kuwa   raia wengi  wamejitokeza barabarani  huku wakishangilia kauli hiyo ya ”Mapinduzi”.
Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.

clouds stream