Monday 4 May 2015

Mayweather apewa ushindi

Mayweather apewa ushindi



 Floyd Mayweather baada ya kutangazwa mshindi.
Floyd Mayweather amemshinda Manny Pacquiao kwa pointi kwenye pambano ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa masumbwi kote duniani, pambano hilo limemalizika muda mfupi kwenye ukumbi wa MGM Grand Las Vegas, Marekani.

Kama ilivyotegemewa na watu wengi, Pacquiao alirusha makonde mengi kwa mpinzani wake lakini Mayweather aliweza kuhimili mikikimikiki ya makonde hayo ambayo yalionekana kuwa mepesi kwake.
Pacquiao akifanya mashambulizi dhidi ya Mayweather
Mayweather aliwashawishi majaji wa pambano hilo kwa kutupa makonde machache lakini mazito yaliyo muingia sawasawa mpinzani wake. Majaji wa mpambano huo wamempa Mayweather ushindi wa pointi 118-110, 116-112,116-112.

Hivi ndivyo mambo yalivyo kua.

clouds stream