Tuesday 26 May 2015

Burundi: Maandamano yapamba moto, basi lachomwa moto

Burundi: Maandamano yapamba moto, basi lachomwa moto

Tarehe May 25, 2015
Maandamano mjini Bujumbura.
Maandamano mjini Bujumbura.
Basi moja la uchukuzi limechomwa moto mjini Bujumbura Burundi na waandamanaji waliorejea mabarabarani kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Waandamanaji wamechoma moto magurudumu  katika eneo la Kanyosha. Kitongoji hicho kimekuwa kitovu cha maandamano hayo dhidi ya awamu ya tatu ya rais Nkurunziza.
Maandamano haya yanarejea baada ya kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani Zedi Feruzi nje ya nyumba yake katika mji mkuu Bujumbura.
Aidha wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha mazungumzo na serikali rais Pierre Nkurunziza ya kutaka kutatua  mzozo ulioko wa kisiasa.
Uamuzi ambao wengi wanasema kuwa unaenda kinyume na sheria na ndio iliyosababisha kuwepo kwa jaribio la kumpindua, na maandamano ya wiki kadhaa.
Hadi sasa tayari zaidi ya raia 100,000 wa taifa hilo wametorokea mataifa jirani ikiwemo nchini Tanzania.

clouds stream