Thursday 4 August 2016

Afariki Kwa Kukanyagwa Na Treni Dar

Tarehe August 5, 2016
PUGUV 1

Mtu mmoja anadaiwa kupoteza maisha baada ya kukanyagwa na treni alipokuwa akijaribu kudandia ikiwa tayari katika mwendo.

Kijana huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja alidondoka wakati gari moshi hilo likiwa katika mwendo katika maeneo ya Kamata Kariakoo akiwa na lengo na kugeuza na treni hilo kwa safari ya kuelekea Pugu.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kijana huyo alidandia treni hilo likiwa kwenye mwendo huku milango ya treni ikiwa haijafunguliwa na kulazimika kuning’inia kwa nje ndipo alipojibamiza katika kingo za treni na kudondoka chini kisha kukanyagwa na kufa papo hapo.


Tukio hilo linatokea ikiwa ni siku chache kupita tangu kuongezeka kwa treni ya pili maarufu kama treni ya mwakyembe na kuongezeka kwa vituo vya kusimama kwa treni hizo kwa ajili ya kushusha na kupakia abiria.

clouds stream