Saturday 13 August 2016

Bonge La U-Turn, Messi Arejea Timu Ya Taifa.

Tarehe August 13, 2016
Lionel Messi.
Lionel Messi.

Nguli wa Soka na Mshindi wa mara 5 wa FIFA Ballon d’ Or, Lionel Messi amepiga bonge la U­turn na kutangaza rasmi kurejea katika timu ya Taifa ya Argentina ikiwa ni miezi michache tu imepita tangu atangaze kustaafu kuicheza timu hiyo baada ya kuvunjika moyo kufuatia kushindwa katika fainali ya Copa America, 2016.

Akiwa tayari amekwishaongea na Kocha mpya wa timu ya Argentina, The Albiceleste Boss, Edgardo Bauza, Messi amefanya uamuzi wa kuiwakilisha nchi yake tena.

“Tayari naona kuna matatizo kibao katika mpira wa Argentina na hivyo basi nisingependa kutengeneza tatizo lingine tena,”amesema Messi katika taarifa maalum aliyoitoa siku ya Ijumaa. 

 Amesema kuwa hataki kusababisha tatizo lolote kwani siku zote amekuwa akifanya kinyume na hilo na kuisaidia timu pale anapoweza.

“Tunatakiwa kurekebisha mambo mengi sana katika mpira wa Argentina lakini ningependa kufanya hivyo nikiwa ndani na sio kupinga nikitokea nje,” amezidi kufunguka Messi.

Nahodha huyo ameweka wazi kuwa ni mapenzi yake kwa Argentina ndio yaliyomshawishi kurudi katika timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia lijalo.

“Mambo mengi sana yalikuwa ndani ya kichwa changu siku ya fainali ya mwisho na kiukweli kabisa nilifikiria kuachana na timu ya Taifa, lakini nalipenda Taifa hili na Jezi ya Argentina,” amesema Mkali huyo anayekiwasha katika klabu ya Barcelona.

clouds stream