Friday 12 August 2016

Shibuda Aifananisha UKAWA Na Mlenda, Amfagilia JPM.

Tarehe August 12, 2016
Katibu Mkuu wa Chama cha ADA-Tadea, John Shibuda. V 1
Katibu Mkuu wa Chama cha ADA­Tadea, John Shibuda.

 Katibu Mkuu wa Chama cha ADA­Tadea, John Shibuda amejitokeza katika mkutano wa Rais, Dkt. John Magufuli katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza na kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa namna ambavyo anatatua kero za wananchi.

Akiwa mmoja wa maelfu ya wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani waliojitokeza kumsikiliza Rais Magufuli akihutubia katika viwanja vya Furahisha, amevitaka vyama vingine vya siasa nchini kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuwa kazi anayoifanya ni kwa ajili ya watanzania wote.

“Mheshimiwa Rais Magufuli endelea kuwahudumia watanzania na nikuambie sijawahi kuona mchongoma unang’olewa kwa upepo au sijawahi kuona utelezi wa mlenda unamwangusha mtu mzima,” amesema.

Shibuda ametoa rai kwa vyama vya siasa vinavyounda UKAWA kuwa vinapaswa kutambua kwamba Rais Dkt. Magufuli ni mtu mzuri ndiyo maana aliwasaidia kumaliza mgogoro wa uchaguzi wa Meya Jijini Dar es Salaam hivyo watambue mchango wake kwa Taifa .

clouds stream