Wednesday 3 August 2016

Madiwani UKAWA Wamvaa Makonda Kwa Dharau

Tarehe August 3, 2016
Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob.
Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob.
 Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob amemshutumu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kudai kuwa ana tabia ya dharau na kutoheshimu viongozi wenzake hasa wa upinzani akiwaona kuwa hawatendi kazi vizuri.
Jacob ametoa kauli hiyo kwa niaba ya madiwani wenzake kutoka UKAWA katika Manispaa ya Kinondoni baada ya madiwani hao kususia kikao kilichoitishwa na Makonda.
Makonda aliitisha kikao cha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara za Manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni pamoja na madiwani wote wakiwemo na wabunge wananounda Halmashauri hizo.
Akijibu tuhuma hizo Makonda amedai kuwa huyo anayelalamika anafanya utoto na kwamba akikua ataacha.
“Narudia tena siyo kazi yangu kuangalia nani hajaja kwenye kikao,” amesema.
Katika kikao hicho ambacho kililenga kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo maeneo yaliyovamiwa, Makonda alitaka kuondolewa kwa maafisa ardhi wa Ilala na Kinondoni.

clouds stream