Wednesday 3 August 2016

MAHAKAMA YAFUTA KESI YA RUSHWA KWA WABUNGE

Tarehe Aug, 4 2016images (36)

V 1
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam imewafutia Mashtaka ya kuomba Rushwa ya Shilingi Milioni 30 yaliyokuwa yanawakabili wabunge Kangi Lugola wa Mwibara, Victor Mwambalaswa wa Lupa na Murad Sadiq wa Mvomero.

Hatua hiyo inakuja baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP, kusema hana nia ya kuendelea na Mashtaka dhidi ya wabunge hao hivyo kuiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia mashtaka wabunge haoKANGIWabunge hao Walikuwa wakituhumiwa kupokea Rushwa hiyo kati ya Machi 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa walimuomba rushwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Gairo, Mbwana Magotta ili watoe mapendekezo mazuri kuhusu hesabu ya fedha za bajeti ya mwaka 2015/2016 za halmashauri hiyo.

clouds stream