Thursday 4 August 2016

Tundu Lissu Atiwa ‘Korokoroni’ Tena.

Tarehe August 4, 2016
cell+pic
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amekamatwa na Jeshi la Polisi kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni kufanya Mkutano wa Hadhara Wilayani Ikungi katika Jimbo lake.
Katika ujumbe alioutoa yeye mwenyewe akiwa chini ya uangalizi wa Polisi Lissu amesema maneno yafuatayo;
Nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara Mji Mdogo wa Ikungi ambao ni Makao Makuu ya Jimbo langu la Singida Mashariki. Mara baada ya kushuka jukwaani nimefuatwa na Regional Crimes Officer wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Regional Police Commander Singida nikamatwe.
“Apparently kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam. Kwa hiyo niko nguvuni na ninasubiri maelekezo ya RPC juu ya wanakotakiwa kunipeleka,” amesema Lissu.
“It’s likely nitasafirishwa Dar usiku huu. In fact ni usiku huu kwa taarifa za sasa hivi. Kwa vyovyote itakavyokuwa, ther’s no turning back. There’s no shutting up. Nitapambana kutetea haki yetu ya kuwasema watawala popote nitakapokuwa, whether in freedom or jail, as long as I’ve a voice to speak with,” amesisitiza Lissu.
Taarifa za kukamatwa kwa Mbunge huyo wa CHADEMA ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, zilithibitishwa na Msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene ambaye alikiri na kudai kuwa ni kweli mbunge huyo amekamatwa na tayari viongozi wa chama mkoani na ngazi ya Taifa wanafuatilia kwa ukaribu kujua sababu ya kushikiliwa kwake na kutoa msaada kasri itakavyowezekana huku akiahidi kuujulisha Umma juu ya suala hilo.

clouds stream