Tuesday 30 August 2016

JWTZ Kufanya Usafi Wa Mazingira Jijini Dar Es Salaam

Tarehe August 30, 2016
KanaliNgemelaV 1
Msemaji wa JWTZ, Kanali Ngemela Lubinga

Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), limesema kuwa litashirikiana na uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam Septemba mosi mwaka huu.

Msemaji wa JWTZ, Kanali Ngemela Lubinga ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia maandalizi ya shughuli ambazo jeshi hilo litazifanya siku hiyo ambapo Jeshi hilo litakuwa linafikia kilele cha maadhimisho ya miaka 52 tangu kuanzishwa kwake.

Kanali Lubinga anasema pamoja na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali shughuli nyingine zitakazofanywa na wanajeshi hao ni za kijamii ikiwemo kushiriki katika zoezi la uchangiaji damu kwenye vituo mbalimbali pamoja na kufanya mazoezi ya ndege za kijeshi. 

clouds stream