Saturday 13 August 2016

JPM Aahidi Kurudisha CCM Ya Mwl. Nyerere.

Tarehe August 13, 2016
Mwenyekiti wa kwanza wa CCM na Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Mwenyekiti wa kwanza wa CCM na Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais, Dkt. John Magufuli amesema anataka kuona CCM mpya na kuahidi kukirudisha chama katika maadili kama kilivyoachwa na Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Amaan Karume.

Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi waliojitokeza kumshuhudia wakati akiingia katika Ofisi Ndogo za CCM Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kushika wadhifa huo wa Uenyekiti Julai 23, mwaka huu, Mjini Dodoma.

Amewataka wanachama wa chama hicho kumvumilia wakati atakapokuwa akifanya kazi ya kukirudisha kwenye maadili, kwani katika kuifanya kazi hiyo mahali atakapoamua kunyoosha, atanyooshea hapo hapo hata kama kuna kigogo ataondoka.

“CCM tumepanga tuanze kujisahihisha, kwa sababu ni chama ninachokipenda nimekulia humu, kilikuwa kimeanza kupoteza dira na hili lazima niliseme wazi bila unafiki,” alikiri Rais Magufuli.

clouds stream