Monday 8 August 2016

Mwigulu Atangaza Kiama Kwa Wasafirishaji Wa Madawa Ya Kulevya

Tarehe August 9, 2016
Screen-Shot-2016-05-23-at-12.51.47-PMV 1

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa maofisa wanaohusika na udhibiti wa dawa za kulevya katika mpaka wa Tunduma, Mkoa wa Songwe, kuwakamata wahusika wa uvushaji wa dawa hizo kutoka nchini kwenda nchi jirani ya Zambia na nyingine zilizopo ukanda huo.

Nchemba amesema ni jambo lisilofichika kuwa kwa sasa Tanzania imechafuka kutokana na kutapakaa kwa dawa za kulevya.

Amesema kutokana na Watanzania wengi kukamatwa katika nchi mbalimbali duniani, wakijihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya, imefikia hatua kwa baadhi ya nchi kufikiria kuongeza masharti zaidi kwa kila atakayejitambulisha kuwa Mtanzania.

“Hatuwezi kuacha nchi ikachafuka kwa sababu tu ya watu wachache.Ukienda China Watanzania zaidi ya 200 wanashikiliwa kwa dawa za kulevya, Pakistan wapo, India, Afrika Kusini ni Watanzania na hili linatuchafua sana,” amesema Nchemba.

Katika hatua nyingine, Nchemba aliutaja mpaka wa Tunduma kuwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa kupitisha dawa hizo na kutaka nguvu kuongezwa zaidi ili kuwezesha misako.

clouds stream