Wednesday 3 August 2016

Bilionea Mo Dewji Amwaga Milioni 100 Ni Ya Usajili Tu.

Tarehe August 2, 2016
Mohammed Dewji "MO" amkabidhi rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva, kiasi cha shilingi, milioni 100 kwa ajili ya usajili.
Mohammed Dewji “MO” amkabidhi rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva, kiasi cha shilingi, milioni 100 kwa ajili ya usajili.

 Bilionea Mohammed Dewji ameanza kazi katika klabu ya Simba baada ya kutoa Sh milioni 100 kusaidia usajili.

Mo ametoa fedha hizo leo na kuzikabidhi kwa Rais wa Simba, Evans Aveva.

Mo alikubali kuisaidia Simba katika usajili wakati mchakato wa kwenda kwenye mabadiliko na kuwa kampuni ukiendelea.

Tayari bilionea huyo kijana ametangaza kumwaga fedha Sh bilioni 20 ili kupata hisa asilimia 51 ya umiliki wa klabu hiyo na wanachama wameridhia katika mkutano wa wanachama uliofanyika juzi Jumapili.

clouds stream