Thursday 12 March 2015

Ajali Basi la Majinja, abiria watoa ya moyoni

Ajali Basi la Majinja, abiria watoa ya moyoni

Watu arobaini na wawili wamefariki dunia huku ishirini na wawili wakiwa wamelazwa hospitalini baada ya ajali ya barabarani iliyotokea asubuhi ya Jumatano, Machi 11, 2015 huko katika eneo la Changarawe, Mufindi katika mkoa wa Iringa.
Ajali hiyo ilitokea baada ya basi la abiria la kampuni ya Majinja Express lililokua likitokea Iringa likielekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori lililokua likitokea Dar es Salaam kuelekea Iringa.
Kwa mujibu wa Mkuu wa polisi katika mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, amethibisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa kati ya watu 41 walioaga dunia, wanaume ni 33, wanawake 5 na watoto watatu.
Akizungumzia chanzo cha ajali hiyo mmoja wa abiria aliyekuwemo katika basi hilo amesema  kwamba dereva wa lori alijaribu kukwepa moja ya shimo katika barabara suala lililomsababisha kutoka katika upande wake wa barabara hadi upande wa basi hilo na kusababisha kugongana na basi hilo la kampuni ya Majinja Express.
Baadhi ya majina ya abiria waliokuwemo katika basi la Majinja   ni kama ifuatavyo:
Baraka Ndone (dereva), Yahya Hassan ( kondakta), Ester Emanuel, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni, Frank Chiwango, Luteni Sanga, Teresia Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana, Catherine Mwate, Mwajengo, Ndulile Kasambala, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala, Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule Dominick Mashauri na Omega Mwakasege.
Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi, Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa Iman Mahenge , Juma Sindu, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule,
Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na Oswald.

clouds stream