Wednesday 4 March 2015

TMA : Tanzania kukumbwa na ukame 2015

TMA : Tanzania kukumbwa na ukame 2015

Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari juu mabadiliko ya   hali hewa  ambapo hali ya hewa kwa mwaka huu nchini  Tanzania  inatarajiwa   kukumbwa  na  upungufu  wa  mvua.
Kwa mujibu wa  Mkurugenzi mkuu wa TMA, Agnes Kijazi amesema kwamba kufuatia  hali ya ukame kutokea mwaka huu, huenda ika athiri uzalishaji wa umeme kutokana na nchi ya Tanzania kutegemea maji kama chanzo cha nishati.
Upungufu wa unyevu ardhini, ukosefu wa mvua umetajwa kuathiri shughuli za kilimo katika maeneo mengi nchini Tanzania.
Akizungumza wakati wa kutoa mwelekeo wa mvua  za masika kwa  marchi, April na Mei mwaka huu Kijazi  amesema  mvua za wastani na juu ya wastani, zitanarajiwa katika baadhi ya maeneo hususani Kanda ya Ziwa Victoria na maeneo ya Kusini.
Kwa upande wa maeneo yanayopata misimu miwili  ya mvua, mvua zinatarajia kuanza mapema  na kutakuwepo kwa vipindi vya ukame katika maeneo mengi hususani machi na Mei.

clouds stream