Monday 16 March 2015

Urais 2015: Machinga wajichanga kumchukulia fomu Lowassa



Urais 2015: Machinga wajichanga kumchukulia fomu Lowassa




Wafanya biashara ndogondogo maarufu kama Machinga wamechangisha fedha kiasi cha shilingi Milioni moja na kumkabidhi mbunge wa Monduli Bw. Edward Lowassa ilia aweze kuchukulia fomu ya kugombea urais nchini Tanzania katika uchaguzi mkuu unatakaofanyika mwezi oktoba mwaka huu.
Aidha kiasi hicho cha fedha kimekabidhiwa na wawakilishi wa umoja wa wamachinga nchini Tanzania hivi karibuni nyumbani kwake Ngarash Monduli. iBaada ya kumkabidhi kiasi hicho cha fedha walimkabidhi pia Ngao na Mkuki ambayo wamesema atatumia katika safari yake ya matumaini.
Uchaguzi mkuu wa rais pamoja na wabunge unatarajia  kufanyika mwezi oktoba mwaka 2015 huku wanasiasa  mbalimbali wakitangaza nia ya kutaka kuingia  katika kinyang’anyiro cha hicho.

clouds stream