Thursday 12 March 2015

TRL: Mabehewa 22 yaliyoagizwa kutoka Korea Kusini ni mapya ?

TRL: Mabehewa 22 yaliyoagizwa kutoka Korea Kusini ni mapya ?

Shirika la Reli Tanzania limekanusha vikali taarifa zilizochapiwa na baadhi ya magazeti kuwa mabehewa 22 ya abiria yaliyonunuliwa na serikali ya Tanzania nchini Korea Kusini ni mabovu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya ofisa uhusiano  wa  shirika hilo imesema kwamba mabehewa hayo yalifanyiwa majaribio na TRL na kuridhika kuwa hayana kasoro yoyote.
Mabehewa hayo yaliwasili nchini Desemba,2014 ambapo shirika hilo lilipeleka maombi katika Mamlaka ya Udhibiti wa Usafrishaji wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) kwa lengo la kuruhusiwa kuanzisha huduma ya treni ya abiria ya Deluxe ambapo pia nauli maalumu itatozwa kwa abiria hao.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa  mabehewa yote yapo ndani ya mkataba ambao umewekwa masharti maalumu ikiwemo masharti ya gharama kwa mtengenezaji kuyafanayia marekebisho endapo hitilafu zitajitokeza wakati wa kipindi cha majaribio.
Mikataba imetoa dhamana ya kati ya mwaka mmoja na miwili kwa ajili kurekebisha hitilafu zozote zitakazojitokeza wakati wa matumizi.
Katika hatua nyingine mabehewa yanatarajiwa kutumiwa katika huduma mpya iliyopewa jina la Deluxe kwenda mkoani Kigoma kuanzia April 1, 2015.

clouds stream