Thursday 12 March 2015

Sakata la Zitto Kabwe kuvuliwa uanachama lachukua sura mpya

Sakata la Zitto Kabwe kuvuliwa uanachama lachukua sura mpya


Sakata la Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuvuliwa uanachama Chadema limechukua sura mpya kufuatia chama cha Chadema kutomwandikia barua ya kuvuliwa uanachama mbunge huyo suala linalopelekea kuendelea na shughuli zake kamati  kama kawaida.
Bunge linasemaje kuhusiana na sakata hilo,
Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  imesema kwamba haijapata barua yeyote kuhusu kuvuliwa uanachama wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Kwa mujibuwa  katibu wa Bunge Dk.Thomas Kashililah amesema kwamba kwa kuwa bado hawajapa barua kutoka Chadema Zitto bado ni Mbunge halali wa Kigoma na anatakiwa kuendelea  na shughuli kama kawaida.
Ameongeza kuwa ikiwa Bunge litapata Barua ya kuvuliwa uanachama, Bunge litafanya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo zinazo mkabili ndipo litoe uamuzi. Hata hivyo amesema si lazima spika akubaliane na uamuzi wa kutengua ubunge wa Mbunge  husika kwani kama haikuwa halali kuvuliwa uanachama Spika hubatilisha uamuzi wake wa kumvua ubunge mhusika.
Naye Ofisa Hbari wa Chadema Tumaini Makene amesema chama hicho kitajitahidi kulifanyia kazi suala hilo kwa kuzingatia sheria na taratibu  pamoja na kuandaa barua hiyo kwa wakati.
Katika hatua nyingine Zitto amesema anachukulia suala la kuvuliwa uanachama  kama changamoto ambayo inazidi kumkuza na kumkomaza katika tasnia ya siasa ndani na nje ya nchi.

clouds stream