Wednesday 11 March 2015

Zitto atoa ya Moyoni kufuatia kuvuliwa uanachama CHADEMA

Zitto atoa ya Moyoni kufuatia kuvuliwa uanachama CHADEMA


Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe  ametoa ya moyoni kufuatia kuvuliwa uanachama CHADEMA. Hatua ya kuvuliwa uanachama wa chama hicho unafuatia Mwanasheria mkuu wa CHADEMA,Tundu Lissu kutangaza rasmi   jana  kumvua  uanachama Mbunge wa  Kigoma  Kaskazini  Zitto Kabwe.
Aidjha, akifafanua  jambo hilo Tundu  Lissu amesema  iwapo mwanachama atafungua kesi dhidi ya chama na iwapo atashidwa atakuwa amejiondoa mwenyewe. Mwaka jana  Zitto  alifungua kesi Mahakama kuu  akipinga kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kumjadili, akikitaka chombo hicho cha sheria, kukielekeza chama chake, kusubiri kwanza rufaa yake aliyokuwa amekata katika Baraza Kuu.
Baada ya kupata taarifa hizo Zitto amesema kuwa   hakuwa  na wito wa mahakamani jana na  Jaji  aliyekuwa  akiisikiliza  kesi  hiyo amehamishiwa Tabora, hivyo  mwanasheria  wake  ameenda  kufuatilia  mazingira  ya  hukumu  hiyo.
“Hatuna taarifa ya Jaji Mpya. Mwanasheria wetu anafuatilia na atatoa statement”, ameandika  Zitto  Kabwe  katika  ukurasa  wake  wa  twitter.
Ujumbe aliouandika Zitto Kabwe katika ukurasa wake wa twitter.

clouds stream