Thursday 12 March 2015

Zaidi ya watu 40 wahofiwa kufariki kwenye ajali Iringa

Zaidi ya watu 40 wahofiwa kufariki kwenye ajali Iringa



Inasadikiwa  watu wapatao 50 wanahofiwa kufa papo hapo baada ya basi  la Majinja Express  kugongana na lori na kuangukiwa na kontena.
Basi hilo ambalo lilikuwa linafanya safari yake kutoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam limegongana na lori la mizigo. Idadi kamili  ya watu  waliodhurika na ajali hiyo bado haijajulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na amesisitiza kuwa  kwa  sasa yuko njiani kuelekea eneo la tukio.

clouds stream