Thursday 12 March 2015

PSG pungufu yaitupa nje Chelsea

PSG pungufu yaitupa nje Chelsea

Mabingwa wa Ufaransa wameonyesha umwamba wao wa kucheza wakiwa pungufu na kuitupilia mbali Chelsea kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Stamford Bridge, Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya 81 na beki kisiki Cahill kabla ya kusawazishwa dakika tano baadae kupitia kwa David Luiz.
Mpira uliendelea kuwa mgumu sana kwa timu zote mbili baada ya PSG kucheza wakiwa nusu kwa kipindi kirefu baada ya mshambuliaji wake matata Zlatan Ibrahimovic.
Chelsea walipata goli la pili kwa njia ya penati ya utata baada ya beki kisiki wa PSG kunawa mpira kwenye eneo la hatari na Eden Hazard akafunga penati hiyo kwenye dakika za nyongeza za mchezo huo baada ya dakika 90 kutoka sare ya 1-1.
PSG awakukata tamaa walipigana na muda baadae dakika ya 114 nahodha mpiganaji Thiago Silva anafunga bao kwa njia ya kichwa, na mpaka mwisho wa mchezo mabao ni 2-2 na PSG anafuzu kwa bao ya ugenini.

clouds stream