Thursday 26 March 2015

Urais 2015: CCM yamuonya Lowassa

Urais 2015: CCM yamuonya Lowassa

Chama cha Mapinduzi CCM kimeibuka na kusema kuwa vitendo vinavyofanywa na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa  ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni za chama  hicho.
Akizungumzia suala hilo Katibu wa Itikadi na uenezi CCM Nape Nnauye amesema kwamba  vitendo anavyo vifanya Lowassa ni kuvunja kanuni pamoja na kiburi, matendo ya wazi ya kampeni bila shaka. Kupitia matendo hayo yanaweza kumpotezea sifa ya kuwa mgombea katika chama hicho.
Ameongeza kuwa Lowassa ni miongoni mwa waliopewa adhabu na CCM mwaka jana kwa kuanza kampeni kabla ya muda huku akisisitiza bado yupo katika uangalizi.
Katika hatua nyingine Lowassa amekuwa anadaiwa akitumia makundi mbalimbali kufanya kampeni kupitia vikundi mbalimbali, vikundi hivyo ni wajasiriamali jimboni Monduli mkoani Arusha, mashehe 50 kutoka wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani pamoja pamoja   na wachungaji.
Makundi hayo yaalifunga safari hadi nyumbani kwa Lowassa Dodoma kumshawishi achukue fomu ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa urais utakaofanyika oktoba 2015.

clouds stream