Thursday 26 March 2015

UVCCM yamuonya Nape ‘kumponda’ Lowassa

UVCCM yamuonya Nape ‘kumponda’ Lowassa

Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoani Arusha, umemuonya katibu wa itikadi na uenezi Nape Nnauye kuchunga kauli zake kufuatia kauli aliyoitoa dhidi ya Edward lowassa.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) MKoani Arusha, Robson Meitinyiki amesema Nape  anapaswa kuelewa chama hicho kilibomoka na  kuwa ni chama cha watu wote na kwa sasa chama kimeanza kuimarika kupitia jitihada za Katibu Mkuu, Abdurahamani Kinana na yeye anaanza kujinyanyua na kutaka kukibomoa.
Ameongeza kuwa  Nape aelewe nyuma ya Lowassa wapo wengi na Arusha wanajipanga kwenda kumshawishi achukue fomu na yeye hapaswi kutoa maneno ya kejeli, kwani kuna kanuni na taratibu za vyama vya kumsimamisha mtu kuwa mgombea, kama ana mgombea wake amtangaze japo lazima apitishwe na chama,siyo mtu mmoja.
Kwa upande wake  Katibu Mwenezi Mkoa wa Arusha, Isack  Joseph, amesema Nape afike mahali achunge kauli zake dhidi ya Lowassa, kwani Lowasa ni mtu mwenye heshima katika nchi hii na alikuwa Waziri Mkuu na kuiletea taifa heshima kubwa.
Kwa upande mwoingine Robson  amesema kama Edward Lowassa anafanya maigizo, ili apendwe na watu, basi wanamshauri mgombea wa Nape afanye maigizo hayo, ili apendwe na watu kwa kufuatwa nyumbani kwake.

clouds stream