Tuesday 24 March 2015

Ugiriki yakumbwa na mzigo wa Madeni

Ugiriki yakumbwa na mzigo wa Madeni



Viongozi wa Ujerumani na Ugiriki wakutana ujerumani kuinusuru ugiriki dhidi ya mzigo wa madeni, huku waziri mkuu mteule wa Ugiriki akitoa onyo juu ya mahitaji muhimu ya msaada wa haraka wa kifedha.
Aidha,  waziri Alexis Tsipras wa Ugiriki amemweleza kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwamba bila msaada mpya wa kifedha kutoka umoja wa ulaya, serikali yake haitaweza kuwa na uwezo wa kulipa madeni yake.
Waziri Tsipras ambaye anafanya ziara yake ya kwanza mjini Berlin alipokelewa na mwenyeji wake kansela Angela Merkel kwa gwaride la kijeshi la katika himaye ya chansela huyo.
Viongozi hao Waziri Mkuu wa Ugiriki na chansela wa Ujerumani wameelezea uhumimu wa nchi zote mbili kufanya kazi pamoja kufuatia mazungumzo ya Berlin kuhusu namna ya kukabiliana na madeni ya Ugiriki.
Kwa upande wake waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras , amesema ni muhimu zaidi kwa Athens na Berlin kufanya mazungumzo ya pamoja kuliko kila mmoja kumzungumzia mwenzake.

clouds stream