Tuesday 24 March 2015

Urais 2015: Obama ataka uchaguzi huru Nigeria

Urais 2015: Obama ataka uchaguzi huru Nigeria


Wananchi  nchini Nigeria  wanatarajiwa kupiga kura jumamosi wiki hii baada uchaguzi huo kuhairishwa mwezi uliopita kutokana na mashambulio ya kundi la Boko Haram.
Akizungumzia uchaguzi huo Rais Obama amesema kwamba Nigeria inapaswa kufanya uchaguzi ulio huru na wa haki.
” Wanigeria  wote wanapaswa kupiga kura zao bila ya vitisho ama wasi wasi . Hivyo natoa wito kwa viongozi wote pamoja na wagombea kuzungumza na wapiga kura wao kwamba vurugu hazina nafasi katika uchaguzi wa kidemokrasia,na hawapaswi kuchochea, wasaidie au kujihusisha na vurugu zozote kabla ama baada ya uchaguzi na wakati wa kuhesabu kura.” Alisema Obama
Nina waomba wanaigeria wote kueleza hisia zenu kwa amani na kuwapuuza wote wanaotoao wito wa kufanya vurugu .
Joto la uchaguzi linazidi kupamba moto nchini Nigeria. Mvutano mkali upo kati ya rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na mgombea wa upinzani Jenerali Muhhamadu Buhari wa APC.

clouds stream