Monday 16 March 2015

Rais wa Zambia afanyiwa upasuaji Afrika Kusini

Rais wa Zambia afanyiwa upasuaji Afrika Kusini


Rais wa Zambia, Edgar Lungu, ameruhusiwa kutoka hospitali ya Afrika Kusini baada ya kufanyiwa upasuaji.
Rais huyo aliyechaguliwa karibuni, ana ugonjwa unaomrejea mara kwa mara, na unao athiri koo yake.
Rais huyo   alilazwa hospitali mjini Pretoria Jumaane mara baada ya  kuzimia katika sherehe za siku ya kimataifa ya wananwake mjini Lusaka.
Kwa upande mwingine Mwezi wa kwanza  alishinda uchaguzi wa rais, na kuchukua nafasi ya Hayati Rais Michael Sata, aliyefariki  dunia oktoba mwaka jana.

clouds stream