Wednesday 11 March 2015

Mama Maria Nyerere atoa ya Moyoni baada ya kuzushiwa kifo

Mama Maria Nyerere atoa ya Moyoni baada ya kuzushiwa kifo


Mjane wa  mke wa Rais wa Kwanza wa Tanzania,Hayati Mw.Julius Nyerere ametoa ya moyoni kuhusiana na  taarifa za uzushi  kusambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii kwamba amefariki dunia.
Akizungumza na Televisheni ya Taifa Mama Maria Nyerere  huku akitabasamu  amesema  huu ni mwaka wa uchaguzi hivyo mambo haya ya uzushi si ajabu.
Mtandao wa Hivisasa pia  ulifanikiwa kuongea na mmoja wa mjukuu wake ambaye alikanusha vikali taarifa hizo  ambapo aliamua kupiga naye picha na kuweka katika mitandao ya kijamii kunanusha taarifa hizo.
Miaka ya hivi karibuni imezuka tabia mbaya ya baadhi ya watu kuzusha  na kusambaza  taarifa za vifo dhidi ya watu mbalimbali nchini Tanzania.

clouds stream