Thursday 26 March 2015

Marekani yabaini mpango wa Al shabaab kuishambulia Uganda

Marekani yabaini mpango wa Al shabaab kuishambulia Uganda

Nchi ya Marekani  kupitia  ubalozi  wa  Marekani nchini Uganda, umesema una taarifa za uwezekano wa kutokea  shambulio la kigaidi nchini humo.
Aidha, taarifa ya ubalozi huo imebainisha kwamba shambulio hilo linaweza kutekelezwa wakati wowote, katika maeneo ambayo raia wa mataifa ya Magharibi na Marekani hukutana.
Katika kipindi kilichopita, kundi la Al-Shaabab lenye makao yake Nchini Somalia, limetekeleza mashambulio Nchini Uganda.
Kwa upande mwingine  nhi ya  Marekani  imetoa tahadhari kwa raia wake wote  waliopo nchini Uganda.

clouds stream