Thursday 12 March 2015

Sakata la Escrow: Wahisani wakubali kuimwagia Tanzania mabilioni ya fedha

Sakata la Escrow: Wahisani wakubali kuimwagia Tanzania mabilioni ya fedha


Benki kuu ya Tanzania
Benki kuu ya Tanzania.
Wafadhili mbalimbali kutoka nje ya nchi watanatarajia kutoa kiasi cha shilingi bilioni 784 ambazo ni asilimia 85 ya fedha zilizobaki kukamilisha bajeti ya mwaka wa huu wa fedha.
Hatua ya wafadhili kutoa kiasi hicho cha fedha inafuatia kuridhishwa na  masharti waliyotoa waki itaka serikali serikali ya Tanzania kuwachukulia hatua vigogo serikalini waliopelekea kupotea kwa fedha za umma katika akaunti ya Tegeta Escrow mwaka jana.
Kwa mujibu wa waziri wa fedha Saada Mkuya akizungumzia utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na wafadhili katika kusaidia bajeti ya serikali mwaka huu, amesema wafadhili hao ikiwemo nchi ya Finland wataanza kutoa dola milioni 44 za Marekani hivi karibuni.
Katika hatua nyingine  Mkuya  amesema  serikali inaendelea  kurejesha mahusiano mazuri na wahisani suala litakalo pelekea  waendelee kutoa  fedha  za  kukamilisha  miradi  mbalimbali ya  maendeleo nchini inayotegemea fedha za wahisani.

clouds stream