Thursday 26 March 2015

Brazil yalipa kisasi, yaichapa Ufaransa 3-1

Brazil yalipa kisasi, yaichapa Ufaransa 3-1


Magoli ya vipindi tofauti ya wachezaji Oscar(40′), Neymar 57′ na Luiz Gustavo 69′ yaliitocha Brazil kulipiza kisasi cha kufungwa na Ufaransa kwenye kombe la Dunia 1998.


Ufaransa ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa beki kisiki wa Real Madrid Raphael Varane kwenye dakika ya 21 kwa njia ya kichwa baada ya kutumia kona ya upande wa kushoto iliyopigwa na  Mathieu Valbuena.


Brazil  walitawala muda wote wa mchezo hasa kwa wachezaji wake machachari Neymar na Oscar huku kwa upande wa Ufaransa mshambuliaji wake muhimu Karim Benzema alibana vilivyo, Ushindi wa Brazil unamfanya Dunga kushinda kwa asilimia 100 tangu achukue kikosi hicho mwezi Julai. Mpaka mwisho wa mchezo Brazil wanatoka kifua mbele kwa mabao 3-1.

clouds stream