Monday 8 February 2016

Watuhumiwa 9 Mbaroni Kwa Kutungua Helikopta Simiyu

Watuhumiwa 9 Mbaroni Kwa Kutungua Helikopta Simiyu

Tarehe February 8, 2016
helikopta
Helikopta iliyotunguliwa siku ya tukio
Jeshi la polisi mkoani Simiyu limewakamata watu tisa waliohusika kutungua helikopta kampuni ya Mwiba na kumuua rubani wa helkopta hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushi amesema watu hao tisa wamekutwa pia na bunduki 32 na meno matatu ya tembo.
“Mtuhumiwa wa kwanza ndiye aliyewataja wenzake na sehemu tutakazoweza kuwapata. Watuhumiwa hawa wamekamatwa katika wilaya za Meatu, Maswa na Kishapu,” alisema Mushi.
Watuhumiwa wote  na vitu vilishokamatwa vimehifadhiwa kituo cha polisi mkoa wa Simiyu.
Wiki mbili zilizopita watu wasiojulikana, waliitungua helikopta iliyokuwa ikifanya doria katika pori la akiba, Maswa baada ya kuwapo taarifa kwamba majangili walikuwa wameua tembo mmoja. Katika tukio hilo, rubani wa helikopta hiyo raia wa Uingereza, Rodgers Gower (37) alikufa, huku mwenzake Nicky Bester wa Afrika Kusini akinusurika.

clouds stream