Thursday 11 February 2016

Rais Magufuli, TFF Watuma Salamu Za Rambirambi Ajali Ya Tanga

Rais Magufuli, TFF Watuma Salamu Za Rambirambi Ajali Ya Tanga

Tarehe February 11, 2016
ajali 3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bi. Mwantumu Mahiza, kufuatia vifo vya watu 11 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyosababishwa na Basi la Kampuni ya Simbamtoto kugongana uso kwa uso na Lori lililobeba mchanga katika eneo la Pandamlima, Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga.
Ajali hiyo imetokea leo tarehe 11 Februari majira ya saa 1:15 asubuhi katika eneo hilo lenye mteremko mkali, ambapo basi hilo lolilkuwa likisafiri kutoka Tanga kwenda Dar es Salaam na Lori la mchanga likiwa linaelekea Kiwanda cha Saruji cha Tanga.
Rais Dkt. Magufuli amewapa pole Ngudu, Jamaa na Marafiki wote waliofikwa na msiba huo na amewataka kuwa wavumilivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu.
“Nimepokea taarifa ya vifo hivi kwa mshtuko mkubwa, na kupitia kwako Mkuu wa Mkoa wa Tanga, napenda kuwapa pole nyingi wote waliofikwa na msiba huu mkubwa na naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo,” alisema Rais Dkt. Magufuli na kuwaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi na kuwapa pole majeruhi wote 29 walioumia katika ajali hiyo na kuwatakia kupona haraka.
Vilevile Rais amewakumbusha watumiaji wote wa barabarani hususani madereva wa vyombo vya moto, kuwa makini watumiapo barabara kwa kuzingatia sharia zote zinazosimamia usalama barabarani ili kuepusha ajali.
Wakati huohuo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa familia ya mwandishi wa habari za michezo nchini Hamis Dambaya kufuatia kufiwa na mkewe, mwanae pamoja mama mkwe wake.
Katika salamu hizo, TFF imempa pole Dambaya kwa msibu huo mzito uliomfika na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini, Shirikisho liko pamoja nao katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo ya misiba hiyo.
Mkewe Hamis Dambaya, mwanane na mama mkwe wake wamefariki katika ajali ya bus la Simba Mtoto iliyotokea leo asubuhi katikati ya eneo na Muheza na Hale wakati wakiwa safarini kuelekea jijini Dar es Salaam wakitokea mkoani Tanga.

clouds stream