Tuesday 23 February 2016

Mchezaji ‘Amlima’ Refa Kadi Nyekundu Nchini Uturuki

Mchezaji ‘Amlima’ Refa Kadi Nyekundu Nchini Uturuki

Tarehe February 23, 2016
Salih Dursun akimuonesha refa kadi nyekundu
Salih Dursun akimuonesha refa kadi nyekundu
Mchezaji wa klabu ya Trabzonspor, Salih Dursun, ametolewa nje ya uwanja kwa kumuonyesha mwamuzi kadi nyekundu wakati wa mechi waliyofungwa mabao 2-1 na Galatasaray katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki.
Tukio hilo lilitokea dakika ya 86 ya mchezo baada ya mwamuzi Denis Bitnel kumuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Luis Cavanda kwa kufanya madhambi ndani ya eneo la hatari.
Wachezaji wa Trabzospor walimzingira mwamuzi kupinga kadi hiyo.
Ni wakati huo ambapo Dursun alimnyang’anya refa kadi nyekundu aliyokuwa nayo na kumuonyesha kadi hiyo hatua ambayo ilipelekea na yeye kufukuzwa uwanjani.
Klabu hiyo ilisalia na wachezaji tisa uwanjani.
Hii sio mara ya kwanza kwa klabu hiyo kuingia katika mizozo na waamuzi, kwani Novemba mwaka jana mwenyekiti wao Ibrahim Haciosmanoglu alifungiwa siku 280 baada ya kuwafungia waamuzi wanne uwanjani kwa kushindwa kutoa penati kwa timu hiyo.

clouds stream