Tuesday 23 February 2016

Muhongo Ataka Matumizi Ya Teknolojia Ya Kisasa Katika Utafiti Wa Mafuta, Gesi

Muhongo Ataka Matumizi Ya Teknolojia Ya Kisasa Katika Utafiti Wa Mafuta, Gesi

Tarehe February 23, 2016
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja Masoko  kutoka kampuni  ya Schlumberger, Abdul Adeshina (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja Masoko kutoka kampuni ya Schlumberger, Abdul Adeshina (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameyataka makampuni yanayojishughulisha na utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta nchini kuongeza kasi ya utafiti kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili sekta ya  gesi na mafuta iweze kukua na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.
Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo alipokutana na kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa vifaa na teknolojia katika utafutaji wa mafuta na gesi ya Schlumberger yenye makazi  yake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili  utendaji kazi wa  kampuni hiyo.
Kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam kilihusisha watendaji kutoka Wizara hiyo pamoja na  taasisi zake  likiwemo  Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) na Mamlaka  ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Alisema  Tanzania kwa sasa ina utajiri mkubwa wa  rasilimali ya  gesi ambayo  itachochea katika  ukuaji wa uchumi wa nchi  kupitia umeme wa uhakika utakaotumika katika viwanda na kuongeza  ajira kwa  vijana wa kitanzania.
Aliendelea kusema kuwa ili  sekta ya gesi na mafuta iweze kuwa na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi, Tanzania inahitaji wawekezaji  watakaowekeza kwa kasi kwa kutumia  teknolojia ya kisasa.
Alisisitiza kuwa serikali ipo tayari kushirikiana na mwekezaji  yeyote mwenye nia ya kuwekeza kwenye sekta ya gesi na mafuta kwa kutumia  teknolojia ya kisasa.

clouds stream