Wednesday 17 February 2016

Raia Wa India Afukuzwa Kazi Kwa Kuwaita Watanzania ‘Nyani’

Raia Wa India Afukuzwa Kazi Kwa Kuwaita Watanzania ‘Nyani’

Tarehe February 17, 2016
ramada
Raia wa India, Dennis Smith ameachishwa kazi katika Hoteli ya Ramada, Dar es Salaam kwa madai ya kuwatukana wafanyakazi wa kitanzania wa ngazi za chini kwa kuwaita nyani.
Smith, ambaye ni meneja wa chakula na vinywaji wa hoteli hiyo, aliwatukana na kuwadhalilisha wafanyakazi hao siku ya Sikukuu ya Wapendanao akiwatuhumu kushindwa kuandaa meza vizuri.
Kutokana na udhalilishaji huo, wafanyakazi wa hoteli hiyo jana waligoma wakishinikiza meneja huyo asimamishwe kazi au wao waache kazi.
Meneja Rasilimaliwatu wa hoteli hiyo, Sebastian Nchimbi alisema tayari Smith ameachishwa kazi kutokana na tukio hilo kwani tabia ya unyanyasaji ya mfanyakazi huyo imekua sugu.
Mwakilishi wa wafanyakazi hotelini hapo, Mathew Misalaba alisema licha ya uongozi wa hoteli kumsimamisha kazi Smith, wamelipeleka suala hilo polisi ili hatua stahiki zichukuliwe.

clouds stream