Tuesday 2 February 2016

Muuaji Kigogo Wa CUF Atoboa Siri Ya Aliyemtuma

Muuaji Kigogo Wa CUF Atoboa Siri Ya Aliyemtuma

Tarehe February 2, 2016
Simon Shilage kijana anayedaiwa kumuua Diwani wa CUF.
Simon Shilage kijana anayedaiwa kumuua Diwani wa CUF.
Kijana mmoja aliyefahamika kwaji  na la Simon Shilage miaka 22 amekamatwa   na jeshi   la Polisi akidaiwa  kushirikiana na mwenzake kumuua Diwani wa kata ya Kimwai huko Muleba Ndg. Faustine Muliga wa chama cha wananchi CUF.
Kwa mujibu wa Chanzo chetu kutoka Muleba kimebainisha kuwa kijana huyo alikamatwa jioni ya jana na wananchi wa kijiji cha Kyota akijaribu kutoroka akiwa na  panga lenye damu alilotumia kumuua diwani Muliga.
Alipohojiwa kwa nini ametekeleza mauaji hao   Simon amekiri kuwa kweli yeye na mwenzie mmoja (hakumtaja jina) ndio waliomuua Mhe. Muliga kwa kumkata mapanga akiwa nyumbani kwake wakati  ana angalia taarifa ya Habari.
Kijana huyo amesema kazi hiyo  ya mauaji  hayo walitumwa na aliyekua mgombea udiwani wa Kata hiyo kwa tiketi ya CCM kwenye uchaguzi uliopita, ambaye alikua mpinzani wa Muliga lakini alishindwa kwenye uchaguzi.
Ameongeza kuwa Mgombea huyo aliwaahidi kiasi cha shilingi milioni 1.5 ikiwa watafanikiwa kumuua Muliga na aliwapa “advance” ya shilingi laki moja na nusu (150,000/=).
Baada ya makubaliano hayo vijana hao walimvamia Muliga nyumbani kwake majira ya saa 2 usiku akiangalia “Taarifa ya Habari” ambapo walimkata mapanga maeneo mbalimbali mwilini mwake kabla ya kutokomea kusikojulikana.
Imeelezwa kuwa Simoni  alikamatwa na wananchi wenye hasira kali ambao walitaka kumuua ambapo wali mkata sikio  na kisha  akaokolewa na Polisi.
Mtuhumiwa  huyo   anashikiliwa kituo cha Polisi Muleba kwa upelelezi, kabla ya kupandishwa Mahakamani kujibu tuhuma za Mauaji.
Mtandao huu umemtafuta aliyekuwa mgombea udiwani anayedaiwa  kuwatuma vijana hao bila mafanikio.
Diwani wa Kimwani, Kagera, Faustine Muliga (CUF) aliyeuawa.
Diwani wa Kimwani,  Faustine Muliga (CUF) aliyeuawa.

clouds stream