Wednesday 17 February 2016

Magufuli Arejesha Jeshi Bandarini

Magufuli Arejesha Jeshi Bandarini

Tarehe February 17, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli.
Raisi John Magufuli ameamuru Jeshi la Polisi kurudi bandarini na kufanya kazi za ulinzi wa bandari pamoja na mita za kupimia mafuta.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alitangaza maamuzi hayo ya Rais jijini Dar es Salaam na kusema huo ni utekelezaji wa kile Rais Magufuli alichokisema mwaka jana wakati akitumbua majipu bandarini.
“Kama wananchi ambavyo watakumbuka, huko nyuma kulikuwa na Kitengo cha Polisi Bandarini ambacho kilikuwa kinasaidia ulinzi bandarini, lakini ikafika mahali ambapo Mamlaka ya Bandari ikafikiri wanaweza kuwa na ulinzi wa kwao, sasa Rais ameamua Polisi warudi bandarini na kufanya kazi za ulinzi kama walivyokuwa wanafanya zamani,” alisema Balozi Sefue.
Tayari Jeshi la Polisi limeshatekeleza agizo hilo la Rais na askari Polisi sasa wanafanya kazi ya ulinzi katika Bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine zote nchini.
Balozi Sefue pia alisema polisi watawajibika katika ulinzi wa mita za kupimia mafuta zilizopo bandarini hapo, ambako hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alienda na akamsimamisha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo, Magdalena Chuwa.

clouds stream