Thursday 11 February 2016

Liverpool Yawaomba Radhi Mashabiki

Liverpool Yawaomba Radhi Mashabiki

Tarehe February 11, 2016
Benteke
Benteke
Wamiliki wa kilabu ya Liverpool wamefutilia mbali ada ya tiketi inayogharimu pauni 77 na kuomba msamaha kuhusu dhiki iliosababishwa na tangazo hilo la malipo mapya.
Maelfu ya mashabiki waliondoka katika uwanja wa Anfield kunako dakika ya 77 katika mechi dhidi ya Sunderland ili kupinga ada hiyo ya kiingilio kwa wale wanaoingia katika eneo jipya la uwanja huo.
Katika kurudisha bei ya awali wamiliki wa kilabu hiyo Fenway Sport waliwaambia mashabiki kwamba ‘wamepata ujumbe’.Tiketi hiyo sasa itauzwa pauni 59.
Mmiliki wa kilabu hiyo John W Henry,mwenyekiti Tom Werner na rais wa FSG Mike Gordon walitoa barua ya wazi wakielezea mabadiliko hayo,kufuatia kile walichokitaja kuwa wiki ya kutatiza.
”Sisi watatu tumeshangazwa na madai kwamba hatuwajali mashabiki wetu,kwamba sisi ni walafi na kwamba tunajaribu kujilimbikizia faida za kibinafsi bila kujali kilabu hiyo,”alisema.

clouds stream