Saturday 20 February 2016

Rwanda Wamfagilia Raisi Magufuli

Rwanda Wamfagilia Raisi Magufuli

Tarehe February 20, 2016
Magufuli+Photo
Raisi wa Tanzania, John Pombe Magufuli
Wafanyabiashara wa Rwanda wamepongeza hatua zilizochukuliwa na Raisi John Magufuli katika bandari ya Dar es salaam kwa kuimarisha ufanisi wa bandari na kukuza biashara baina ya Tanzania na nchi jirani.
Hayo yameelezwa na waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa afrika mashariki,kikanda na kimataifa, balozi Agustine Mahiga alipotua nchini akitokea Kigali, Rwanda.
Balozi Mahiga alisema wafanyabiashara hao wamesema tangu raisi Magufuli aanze kuchukua hatua hizo, mizigo yao imekua salama zaidi na wamefanikiwa kuipata kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa awali ambapo mizigo mingi ilikua ikipotea.
Alisema pia raisi wa nchi hiyo, Paul Kagame amemhakikishia kuwa ataendelea kushawishi wafanyabiashara wake kutumia bandari ya Dar es salaam ili kukuza uhusiano wa kibiashara uliopo.

clouds stream