Saturday 6 February 2016

Leicester Noma Wamchapa Man City 3-1,Huth Atupia Mbili

Leicester Noma Wamchapa Man City 3-1,Huth Atupia Mbili

Tarehe February 6, 2016
Danny Drinkwater,Riyad Mahrez wakishangilia na  Robert Huth baada ya Huth kufunga
Danny Drinkwater,Riyad Mahrez wakishangilia na Robert Huth baada ya Huth kufunga
Leicester City sasa wamekuwa gumzo la ligi kuu ya uingereza baada ya wiki iliyopita kuitandika Liverpool magoli mawili kwa bila leo kipigo kimehamia Manchester City kwa kupokea magoli matatu kwa moja.
Leicester walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia mchezaji wake Robert Huth dakika ya 3 baada ya kupokea mpira mrefu uliopigwa nyuma na mabeki wa Man City kuchanganyana.
Hadi mapumziko Leicester walikuwa mbele kwa goli moja na kipindi cha pili raia wa Algeria Riyad Mahrez aliipatia Leicester goli la pili dakika ya 48  na dakika ya 60 Robert Huth akaifungia tena huku Sergio Aguero akiipatia Man City goli la kufutia machozi dakika ya 87

clouds stream